Watuhumiwa wa mauaji ya aliyrekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Jwani Mwaikusa wakiiingizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana Kusomewa Mashtaka yao.(Picha na Yusuf Badi wa Habari Leo).
--
Aidha, watu hao, Joseph Machoche na Jackson Wambura pamoja na wenzao wawili, walisomewa kesi nyingine 10 kwa mahakimu tofauti katika mahakama hiyo; tatu kati ya hizo ni za mauaji pamoja na wizi wa kutumia silaha.
Washitakiwa wengine ni Hassan Wangi na Charles Hembele.
Machoche na Wambura walidaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Gabriel Mirumbe na Wakili wa Serikali Anne Malipula, kuwa Julai 13, mwaka huu saa 4.40 usiku walimuua Mwaikusa.
Siku hiyo hiyo saa 4.45 walidaiwa kumuua Daudi Mwasanjara na saa 4.50 walimuua John Mtui huko Salasala, Dar es Salaam.
Washitakiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa kua mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi ya mauaji bali mahakama kuu na kesi hiyo kupangwa kutajwa Agosti 10, mwaka huu

0 comments:
Post a Comment