Na Stella Chipanha- Bunge-Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewahakikishia wananchi wa Urambo luwa Serikali iko mbio kuanza ujenzi wa barabara kutoka Tabora mjini hadi Urambo kwa kiwango cha lami. Hatua hiyo inalenga kuwaondolea kero ya muda mrefu iliyokuwa inawakabili wakazi wa Wilaya hiyo.
Kikwete alitoa kauli hiyo juzi wilayani Urambo kwenye sherehe fupi za ufunguzi wa Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki iliyogharmu shilingi milioni 170 wakati akijibu ombi la Mbunge wa Urambo Mashariki Samwel Sitta la kuomba barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tabora hadi Urambo. Alisema hadi hivi sasa wakandarasi wawili wameshapatikana na wanawatarajia kuanza kazi mara baada ya makabidhiano maaalum.
Rais Kikwete alifafanua kuwa ili kazi hiyo iende haraka na kama ilivyopangawa wakandarasi hao wamegawana maeneo ambapo wa kwanza atajenga kipande cha kutoka Tabora mjini hadi Ndono na mwingine ataendelea na shemu iliyobaki kutoka Ndono hadi Urambo.
Aliongeza kuwa lengo la Serikali yake ni kuhakikisha mikoa yote inaunganishwa na barabara zilizojengwa kwa kiwango cha lami. Hata hivyo alisema kuwa zoezi hilo litazingatia uwezo wa kifedha wa Serikali kwa kuwa ujenzi wa barabara za kiwango cha lami unahitaji fedha nyingi.
Awali Mbunge wa Urambo Mashariki alisema kuwa barabara hiyo ni muhimu kwani ni tegemeo kubwa kwa wakulima wa tumbaku. Aliongeza Wilaya ya Urambo ni miongoni mwa Wilaya zinazoongoza kwa kulingizia taiafa fedha nyingi za kigeni kutokana na kilimo cha tumbaku , hivyo kuwepo kwa barabara duni kumesababisha wakulima kuzalisha tumbaku kidogo kwa kuwa pembejeo zimekuwa zikichelewa kwa sababu ya barabara.
.jpg)





0 comments:
Post a Comment