MJADALA WA UCHUMI NA FEDHA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM!!

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Bw. Ephraim Mafuruakichangia mada katika semina ya mjadala wa mambo ya uchumi na fedha uliofanyika mwishoni mwa wiki Chuo Kikuu Cha Dar es salaam, Kitivo Cha Biashara , ambapowasomi na wahadhiri kutoka chuo hicho na wataalamu mbalimbali wa mambo yabiashara walikutana,semina hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Nyumba Nchini (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu (kulia) akijadili jambo na Mwakilishi wa Benki ya DuniaNchini Bw. David Robinson mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika kwa mjadala wa mamboya uchumi na fedha uliyofanyika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam, Kitivo chaBiashara na kuhudhuriwa na wataalamu mbalimbali wa masuala yabiashara,ambao walijadiliana changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta zabiashara nchini, na kudhaminiwa na kampuni ya Simu za mkononi ya VodacomTanzania, katikati ni Justin David.

Mwakilishi wa Benki ya Dunia(IMF) nchini Bw. David Robinson akitoamada katika Mjadala wa uchumi na fedha uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar essalaam, Kitivo cha Biashara na kukutanisha wasomi na wataalamu wa mambo yabiashara kutoka Serikalini, Makampuni na Taasisi mbalimbali za Kimataifa,washa hiyo ilidhaminiwa na Vodacom Tanzania.

Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada kwa umakini zilizokuwazikitolewa na wataalamu katika mjadala wa uchumi na fedha, Chuo Kikuu ChaDar es salaam, Kitivo Cha Biashara , ambapo wasomi na wahadhiri kutoka chuohicho na wataalamu mbalimbali wa mambo ya biashara walikutana,na kudhaminiwana Vodacom Tanzania,jana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment