Miss Tanzania 2010 Miriam Gerald wa pili kutoka kulia akizungumza na warembo wanaoshiriki katika shindano la Miss Higher Learning 2010 wakati wa mazoezi yao, yanayofanyika kwenye ukumbi wa klabu ya Billicanas jana jioni.
warembo hao wanatarajia kupanda jukwaani kesho kwenye Viwanja vya Karimjee mjijini Dar es salaam katika shindano hilo linalikutanisha washiriki 12 kutoka vyuo vinne ambavyo ni CBE, IFM,USTAWI na UDOM.
Katika shindano hilo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao ni Ngwear, Quick Raqa na Suma Lee wote kutoka jijini Dar es salaam.
Shindano hilo limedhamini wa na Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom ambao ni wadhamini wakuu wa shindano la Miss Tanzania , Redds Premium Cold, Fabak Fashion, Mustafa Hassanali couture, Vayle Spring na Clouds Fm na kiingilio ni shilingi 5000 tu na hakuna burudani nyingine yoyote ya urembo jijini Dar es salaam kwa siku ya kesho, katika picha kulia ni mmoja wa walimu wa warembo hao Torry.
IFM, USTAWI, CBE, NA UDOM KUUMANA KESHO KARIMJEE!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment