WAKAZI wa Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam, leo walizua kizazaa baada ya kuifunga barabara kuu inayotoka Mbuyuni kuelekea eneo hilo kufuatia gari aina ya Toyota Hiace linalofanya shughuli za daladala kati ya Kunduchi na Mwenge kuwagonga na kuwaua watoto wawili wa familia moja. Vurugu hizo zilisababisha askari wa kutuliza ghasia FFU, kutumia mabomu ya kutoa machozi ingawa baadaye walikatazwa kutumia mabomu hayo na askari wa JWTZ wa kambi iliyopo jirani na eneo hilo kutokana na muingiliano wa mionzi kati ya mabomu hayo na vifaa vyao. Picha kwa hisania ya http://www.globalpublishers.info
HUU NDIYO MTITI WA KUNDUCHI BAADA YA WATOTO KUGONGWA NA KUFA!!
Posted by
ADMIN
You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)








0 comments:
Post a Comment