Leo nilihudhuria kwenye mkutano wa wanahabari na kundi la muziki wa Samba na Capoeira ambalo ni mchanaganyiko wa wasanii kutoka Brazil na Mozambique na walielezea mambo mengi kuhusu muziki huo na kuutangaza nchini Tanzania huku wakisisitiza kushirikiana na kubadilishana utaalamu wa muziki wa Kitanzania na wa Kibrazil.
Wakati huo wote mie nilikuwa bize na Laptop yangu ili kuihabarisha jamii ya kitanzania na ya kimataifa pia juu ya tukio hilo la burudani ambalo linafanyika nchini kwetu likihusisha mataifa matatu yaani Tanzania Brazil na Mozambique.
Nilipomaliza kazi yangu ilibidi niwaonyeshe jamaa habari yao na walionekana kuvutiwa sana na habari hiyo kitu ambacho kilimfanya mmoja wa wasanii wa kundi hilo Bw. Flavio kutoka Brazil kunielekeza zaidi kuhusu muziki huo wa Brazil huku wasanii wenzie na baadhi ya wanahabari Wakishuhudia.
Kwa kunisaidia zaidi akaamua kunielekeza jinsi ya kuupata mtandao wa nchi hiyo unaojihusisha na muziki huo kama unavyomuona akitoa maelekezo zaidi, amesema ukitaka kupata zaidi habari za muziki wa Samba na Capoeira kutoka Brazil unaweza kutembelea kwenye mtandao wa www.abadacapoeira.com.br na kupata habari zaidi kuhusu muziki huo





0 comments:
Post a Comment