CLIFORD NDIMBO ALA SHAVU TENA KLABU YA SIMBA!!

Baada ya Cliford Ndimbo kumaliza muda wake wa miezi mitatu katika klabu ya SIMBA na kuondoka katika kiti cha usemaji wa klabu hiyo ,sasa klabu ya SIMBA imemrejesha msemaji huyo kuendelea na kazi yake kama awali.

Mwenyekiti wa SIMBA RAGE amesema kamati ya utendaji imekaa na kuamua kumrudisha NDIMBO katika nafasi yake kwa muda wa miezi sita kwa uangalizi kama atafanya vizuri watampa mkataba zaidi, lakini akishindwa kufanya vizuri ndani ya miezi sita ataondolewa katika nafasi hiyo. lakini sisi FULLSHANGWE kwa maoni yetu tunaona Ndimbo anafaa kwa nafasi hiyo kwanbi alifanya vizuri katika kipindi chga miezi mitatu aliyokuwa akishikilia nafasi hiyo.

Na ndiyo maana amerejeshwa tena kuwa msemaji wa klabu ya Simba kwani amekuwa siyo mchoyo kwa kutoa habari na ni mtu mwenye ushirikiano mzuri wakati unapohitaji habari kutoka kwa klabu hiyo hivyo tunakutakia kila mafanikio kwa mara nyingine tena katika utumishi wa nafasi hiyo. Kwa hisani ya
www.janejohn5.blogspot.com.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment