Breaking Newwwsssss, Wanafunzi waandamana!!

Habari zilizotufikia hivi punde zinasema wanafunzi watatu wa shule ya Msingi Mtakuja na Kunduchi zilizopo Kunduchi Mtongani ambao majina yao hayakufahamika wamegongwa na kufa hapohapo na gari mambalo namba zake pia hazikupatikana mara moja.

Mpaka sasa wanafunzi na wazazi eneo hilo wameamua kuandamana kitu kilichopelekea jeshi la poilisi kuelekea huko kuzima maandamano hayo, inaelezewa kwamba mambomu ya machozi yametumika ili kudhibiti fujo hizo

Lengo la maandamano hayo ni kwamba wanafunzi hao wanadai eneo la kuvuka wanafunzi hao liwekewe matuta ili kudhibiti madereva wasio waangalifu ambao wamekuwa wakisababisha vifo na majeruhi kwa wanafunzi shuleni hapo, katikatukio hilo kuna watu ambao wanadaiwa kuchochea maandamano hayo wamewekwa chini ya ulinzi na kupakiwa kwenye magari ya polisi

Habari zaidi za tukio hilo tutawaletea baadae.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment