Wagombea wa udiwani katika kata ya Mtoni kutoka kulia ni Ally Ramadhan Chaulembo, Maalim Hassan Mango.Khamis Slim Khamis, Juma Chacha na Ramadhan Dallo ammbao walishuhudia sakata hilo la kuhujumiwa na mwenzao baada ya kuwanasa baadhi ya makada wa chama wakifanya mkutano wa kumpigia kampeni mmoja wa wagombea ambaye walimtaja kwa jina la Ally Shaban Kinyaka anayetetea kiti hicho baada ya kumaliza muda wake wa miaka mitano katika uongozi.
Kwa kawaida taratibu za uchaguzi ndani ya chama cha Mapinduzi wagombea wote wanatakiwa kuongozana pamoja wakati wa kujinadi kwa wapiga kura wao ili kuweka usawa kwa wagombea wote.
Polisi walifika kwa wakati katika eneo hilo lililoko Mtoni Sabasaba na kutumia busara zake kwa kuwaagiza viongozi wa chama waliokuwepo hapo kuorodhesha majina ya watuhumiwa na kuhakikisha wanapeleka taarifa katika ngazi zinazohusika kichama ili watuhumiwa waweze kuchukuliwa hatua ndani ya chama kwa kuwa kosa hilo ni la ndani ya chama zaidi hivyo ni muhumu watuhumiwa wakashughulikiwa na chama.
Mzee Mnali ambaye ni mwenye nyumba anayedaiwa kuwakusanya wajumbe hao nyumbani kwake na kuendesha mkutano huo kinyume na taratibu na kanuni za uchaguzi ndani ya chama cha Mapinduzi CCM kulia ni mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Ibrahim Mwita na kushoto ni mmoja wa wagombea Ramadhan Dallo ambaye pia Mwenyeikiti wa vijana kata ya Mtoni.
Mmoja wa akina mama waliokamatwa katika sakata hilo akitolewa ndani ya nyumba walimokuwa wamejificha baada ya kujifungia ndani.
Mmoja wa akina mama waliokamatwa katika sakata hilo akitolewa ndani ya nyumba walimokuwa wamejificha baada ya kujifungia ndani.
Mmoja wa wagombea na ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM Wilaya ya Temeke Khamis Slim Khamis akiwahoji watuhumiwa waliokaa chini ambao ni Said Shekha kulia Katibu wa Vijana kata ya Mtoni na Hamad Mussa Katibu wa Siasa na Uenezi tawi la sabasaba
Katibu wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya ya Temeke Khamis Slim Khamis akizungumza kwa ukali na mmoja wa watuhumiwa walioshiriki katika mkutano huo wa kampeni Bw. Said Shekha
Katibu wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Wilaya ya Temeke Khamis Slim Khamis akizungumza kwa ukali na mmoja wa watuhumiwa walioshiriki katika mkutano huo wa kampeni Bw. Said Shekha
0 comments:
Post a Comment