Baada ya kufungua maonyesho Rais Luiz Da Silva akaribishwa ikulu na mwenyeji rais Kikwete!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Luiza Lula Da Silva wakiingia ikulu jijini Dar es Salaam na kulakiwa na baadhi ya wakazi waliojitokeza kumpokea jana mchana
(Picha na Fredy Maro).

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha umahiri wake wa kupiga ngoma wakati alipomkaribisha Rais Luiz Lula da Silva wa Brazil(kushoto) ikulu jijini Dar es Salaam jana mchana.

Rais Luiz Lula Da silva wa Brazil akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete jezi namba 9 iliyosainiwa na Mwanasoka nyota wa timu ya Brazil Ronaldo de Lima jana mchana ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini ya NSSF Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Hidegard Mzirai akipokea kikombe cha ushindi wa jumla katika maonyesho ya 34 ya biashara ya kimataifa kutoka kwa marais Jakaya Kikwete wa Tanzania na Luiz Da Silva wa Brazil mara baada ya rais wa Brazil kuyafungua rasmi jana katika viwan ja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam. (Picha na Mwanakombo Jumaa Maelezo)

Rais Jakaya akipeana mikono na rais wa Brazili Luiz Da Silva jana baada ya kukabidhiwa kitabu wakati wa mkutano wa wafanyabiashara na marais hao.




Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wafanyabiashara mbalimbali nchini ambao ulikuwa maaluum kwaajili ya kukutana na rais wa Brazil.

Jakaya Kikwete na mwenyeji wake Rais Luiz Inacio Lula Da Silva wa Brazil wakitazama vifaa mbalimbali katika Banda la Jakaya Mrisho Kikwete ikiwa ni sehemu ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya maonyesho ya Mwalimu Nyerere Jijini Dar-Es-Salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja Mkazi wa Brazafric nchini Tanzania Bw. Readou Sakwa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment