WACHEZAJI WA MPIRA WA KIKAPU WAPIGWA MSASA JIJINI DAR ES SALAAM!!


Mratibu wa Mambo Basketball ameandaa mafunzo kwa makocha, waamuzi na wachezaji wa mpira wa kikapu kwa wanaume na wanawake.
Mafunzo hayo yanafanyika katika uwanja wa international school of Tanganyika (IST) Masaki ambapo yalianza tarehe 13/06/2010 na yatafikia tamati wiki hii tarehe 18/06/2010.

Mafunzo hayo yanawahusisha waalimu wote wa mpira wa kikapu na waamuzi toka hapa jijini Dar es salaam na mikoa ya jirani, Na kwa upande wa wachezaji ni wale waliochaguliwa kipaumbele kikiwa ni wachezaji wa timu ya mkoa wa DSM.

"Tulikuwa tukimtarajia kocha Cutris Symonds wa Hoop Magic Sports Academy toka marekani kuja kushirikiana na makocha wa mambo basketball kutoa mafunzo hayo lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu huenda mpaka mwisho wa semina hii atakuwa hajafika" Amesema Bahati Mgunda

Kwa upande wa Makocha na waamuzi mada kubwa zinazojadiliwa ni majadiliano juu ya ufundishaji /uchezeshaji utakao msaidia mchezaji na kumuendeleza kuutumia ujuzi wake uwanjani pia kumsaidia kimaisha awapo nje ya uwanja (positive coaching/ officiating).
Wachezaji watafundishwa mbinu za uchezaji ki-timu (tactics).

Mambo basketball imekuwa ikifanya mafunzo kwa wachezaji hapa Tanzania katika kuendeleza na kukuza mchezo wa mpira wa kikapu hapa Tanzania. Mbali na Dar es salaam mafunzo mengine yamefanyika katika mikoa ya mikoa ya Morogoro na Dodoma.
Imetolewa na
Coach BAHATI MGUNDA Pichani Mratibu wa MAMBO BASKETBALL

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment