Serikali imesema kuwa, ujenzi wa hospitali ya mkoa wa Mara ulionza tangu mwaka 1975 sasa utarudishwa mikononi mwa Mamlaka ya Askofu wa Jimbo la Musoma kama ilivyokuwa hapo awali.
Akitoa kauli hiyo Bungeni jana, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Prof. David Homeli Mwakyusa wakati akijibu baadhi ya hoja zilizotolewa na Waheshimiwa wabungwe wakati wakijadili Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011.
Akijibu hoja hiyo Mhe. Kawambwa amesema, Kanisa Katoliki limepewa ruhusa ya kuendelea na ujenzi huo kama lilivyoomba tangu mwaka 2007 na kwamba masuala ya fidia kwa wananchi walioathirika kutokana na ujenzi wa hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kubomolewa nyumba zao
Wakati huo huo, Waziri Kawambwa amezitaka Halmashauri zile ambazo hazijateua waratibu wa UKIMWI kufanya hivyo mapema na taratibu za kuiwaajiri waratibu hao zifanyike.
Akijibu hoja za Waheshimiwa wabunge, Mhe. Kawambwa amesema, jumla ya shilingi Bilioni 5.8 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi wa hospitali ya mkoa wa Singida. Amesema, hadi sasa kiasi cha shilingi Bilioni 2 zimekwishapatikana. Amezitaka Halmashauri kuibua harakati za ujenzi wa zahanati zenyewe na Serikali iko tayari kuunga mkono juhudi za Halmashauri hizo ili kukamilisha ujenzi wa zahanati.
Waziri Mwakyusa amesema, hali ya upatikanaji wa dawa katika hospitali na zahanati kwa sasa ni nzuri baada ya Serikali kubadili mfumo wa uagizaji wa dawa hizo kwa 'kits'. Amesema kuwa, kwa sasa kila Mganga wa hospitali, ataagiza dawa kulingana na mahitaji ha mahali hospitali ilipo.
0 comments:
Post a Comment