Mwandishi mmoja wa habari wa gazeti binafsi amepigwa risasi na kuuwawa nje ya nyumba yake huko Kigali mji mkuu wa Rwanda.
Walioshuhudia wamesema mwandishi huyo, Jean Leonard Rugambage, ambaye alikuwa kaimu mhariri wa gazeti la Umuvugizi alipigwa risasi na watu wawili ambao baadaye walitoweka kwa gari.
Walioshuhudia wamesema mwandishi huyo, Jean Leonard Rugambage, ambaye alikuwa kaimu mhariri wa gazeti la Umuvugizi alipigwa risasi na watu wawili ambao baadaye walitoweka kwa gari.
Hivi karibuni serikali ya Rwanda iliagiza kusimamishwa kwa uchapishaji wa gazeti hilo, na likaanza kuandika habari kwenye mtandao.
Uchunguzi
Polisi wamesema hawajui nani aliyefanya mauaji hayo, lakini mhariri mkuu wa gazeti hilo ambaye yuko uhamishoni, Jean Bosco Gasasira, ameilaumu serikali.
Uchunguzi
Polisi wamesema hawajui nani aliyefanya mauaji hayo, lakini mhariri mkuu wa gazeti hilo ambaye yuko uhamishoni, Jean Bosco Gasasira, ameilaumu serikali.
Gasasira ambaye alitorokea Uganda mwezi Aprili baada ya gazeti lake kusimamishwa, na anadai serikali ya Rwanda ilipanga mauaji ya mwandishi Rugambage.
Amedai kwamba ana uhakika mwandishi huyo alipigwa risasi na kuuawa na maafisa kutoka idara ya usalama wa taifa.
Amedai kwamba ana uhakika mwandishi huyo alipigwa risasi na kuuawa na maafisa kutoka idara ya usalama wa taifa.
Gasasira amesema mauaji hayo yametokana na taarifa zilizochapishwa kwenye tovuti ya gazeti la Umuvugizi kuhusiana na jaribio la mauaji ya ya mkuu wa zamani wa jeshi la Rwanda, Luteni Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa nchini Afrika Kusini, mwishoni mwa wiki iliyopita.
Serikali ya Rwanda imeshakanusha kuhusika na kupigwa risasi kwa Luteni Jenerali Nyamwasa. Mkuu huyo wa zamani wa jeshi alikimbilia nchini Afrika Kusini mapema mwaka huu baada ya kutofautiana na Rais Paul Kagame, akimlaumu Rais huyo kwa ufisadi. kwa habari zaidi tembelea www.bbcswahili.com
0 comments:
Post a Comment