Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga Jamal Malinzi akiongea na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotoa mapendekezo yake juu ya marekebisho ya rasimu ya katiba ya Yanga kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa timu hiyo uanaotarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini Dare es salaam kwenye ukumbi wa Police Officers Mess.
Jamal Malinzi ametoa moja ya mapenddekezo yake kuwa Yanga wanatakiwa kuwa na kamati yao ya rufaa itakayomaliza matatizo yao hapohapo klabuni badala ya mtu kutoka nje kuwachagulia viongozi kama ilivyotokea kwa timu ya Simba hivi karibuni ambapo kamati ya uchaguzi ya Simba ilimpitisha Zakaria Hanspope kugombea Uenyekiti wa klabu hiyo lakini kamati ya Rufaa ya TFF ikamkata jina lake.
Hata hivy Simba wamemchagua tena Zakaria Hanspope kwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu hiyo lakini sijasikia TFF wakitoa tamko lolote juu ya hilo kwa hiyo hiyo ndiyo picha ninayoiona na ndiyo mambo ambayo sitaki yatokee ndani ya Yanga, Lakini wanachama wa Yanga wanayo haki ya kuyakubali mapendekezo yangu au kuyakataa huo ni uamuzi wao.
0 comments:
Post a Comment