Mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana ya shirikisho la soka hapa nchini Alhaji MSAFIRI MGOI amesema ratiba ya michuano ya mwaka huu imetolewa kisasa ikiwemo kuzitofautisha timu zinazotoka ukanda mmoja.
Kwenye mchezo wa ufunguzi mabingwa watetezi MJINI MGHARIBI watacheza na KINONDONI kwenye dimba la UHURU jijini DAR ES SALAAM wakati washindi wa pili wa michuano hiyo ya mwaka jana TABORA wao watacheza na PWANI siku hiyo hiyo kwenye dimba la KARUME.
Jumla ya timu 28 zinashiriki michuano hiyo ya mwaka huu ambayo itafikia tamati JULAI 10 siku ambayo itachezwa michezo wa fainali kwenye dimba la UHURU hapa jijini DAR ES SALAAM.
Habari kwa hisani ya http://www.janejohn5.blogspot.com/





0 comments:
Post a Comment