Mwanamuziki mkongwe wa Afrika Kusini Yvonne Chaka Chaka(kushoto) ambaye pia ni Balozi wa Kimataifa katika Mapambano dhini ya Malaria Duniani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya kutokomeza Malaria Duniani yenye kauli mbiu “Tuungane Kutokomeza Malaria” leo katika shule ya Msingi Uhuru Wasichana jijini Dar es salaam.Pamoja na na mambo mengine balozi na mwanamuziki huyo amehimiza ushiriki wa jamii nzima hasa wanafunzi kupitia shule zao kupewa elimu kuhusu Malaria kupitia michezo mbalimbali, Kulia ni Bi. Anna McCartney-Melstad Mshauri wa “Voices for Malaria Free Future II – Tanzania kutoka Chuo cha Afya ya Jamii Bloomberg.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mwanamuziki mkongwe wa Afrika Kusini Yvonne Chaka Chaka(katikati) ambaye pia ni Balozi wa Kimataifa katika Mapambano dhidi ya Malaria Duniani akisisitiza jambo kuhusu mchango wake katika mapambano dhidi ya Malaria katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania na namna nchi za Afrika zilizochini ya Jangwa la Sahara zinavyoweza kuungana kutokomeza ugonjwa wa Malaria leo katika shule ya Msingi Uhuru Wasichana jijini Dar es salaam.Kushoto ni Bw. Godfrey Boniface Afisa kutoka Right to Play Tanzania na kulia ni Bi. Anna McCartney-Melstad Mshauri wa “Voices for Malaria Free Future II – Tanzania kutoka Chuo cha Afya ya Jamii Bloomberg
Mwalimu Maua Rashidi wa Shule ya Msingi Uhuru Wasichana ya jijini Dar es salaam akiwaandaa baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo kushiriki michezo mbalimbali leo shuleni hapo wakati wa kampeni ya kutokomeza Malaria nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa wanafunzi wa shule hiyo kupitia michezo.
0 comments:
Post a Comment