WAMBURA ANAWEZA KUFUNGIWA NA TFF ENDAPO ATAENDA MAHAKAMANI!!

Mwenyekiti wa kamati ya Sheria , Maadili na Hadhi za Wachezaji Alex Mgongolwa kulia akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Mpira Tanzania TFF Karume Jijinbi Dae es salaam kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF Fredirick Mwakalebela.
Richard Wambura mgombea aliyeondolewa kwenye uchaguzi wa Simba unaotarajiwa kufanyika Mei 9 mwaka huu akizungumza na wanahabari baada ya kupata taarifa za kondolewa kwa jina lake.

Mwenyekiti wa kamati ya Sheria Maadili na Hadhi za wachezaji wa TFF Alex Mgongolwa leo ametolea ufafanuzi mbalimbali katika masuala ya kisheria yanayohusu wanachama wa FIFA, CAF, SECAFA na hatimaye TFF wakati alipozungumza na waandishi wa habari juu ya kauli mbalimbali ziliotolewa baada ya Richard Wambura aliyekuwa mgombea katika uchaguzi wa klabu ya Simba kuenguliwa na kamati ya Rufaa ya TFF hivi karibuni.

Richard Wambura alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuna mchezo mchafu dhidi yake unaofanywa na TFF na anafikiria kuitafuta haki yake mahali pengine hata hivyo hakusema kama ataenda mahakamani.

Akizungumzia sakata hilo Alex Mgongolwa amesemamsimamo wa fifa kuhusu migogolr ya kimichezo uko wazi ni kwamba mwanachama wa FIFA kamwe haruhusiwi kupeleka mgogoro wa kimichezo katika mahakama za kawaida za nchi hii ni kwa mjibu wa ibara ya 64(2) ya katiba ya fifa.

Hivyo TFF kama mwanachama inawajibika kutimiza wajibu huu chini ya ibara ya 13(1). (d) wajibu huu unaihusu TFF na wanachama wake kuheshimu katiba, kanuni na maagizo ya FIFA.

Sanjali na Hayo TFF katika katiba yake ibara ya 1(6) imeeleza bayanainawajibika kuheshimu katiba ,kanuni, maagizo na maamuzi ya fifa na kuwataka wanachama wake kwa mujibu wa katiba yake ibara ya 12(1) (d) kuheshimu katiba kanuni maagizo na maamuzi ya FIFA,CAF,SECAFA na TFF.

Kwa mujibu wa ibara ya 12(2) (e) na ibara ya 70 ya katiba ya TFF ni marufuku kupeleka mgogoro wa kimichezo katika mahakama za kawaida za nchi badala yake kuna mahakama ya kimichezo ya CAS inayoweza kutatua migogoro hiyo.




Kutoheshimu wajibu huu wa kikatiba kutasababisha mwanachama kufukuzwa uanachama wake kwa TFF, SECAFA, CAF au FIFA.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment