TAWLA KUADHIMISHA MIAKA 20 YA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO!!

Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) Maria Kushonda akizungumza na waandishi wa habari jijini leo kuhusu kuadhimisha miaka ishirini (20 yrs) ya utetezi na kuungamkono haki za Wanawake na watoto. siku ya tarehe 10 Mei,2010 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Katika sherehe za maadhimisho hayo TAWLA itaungana na Rais Jakaya Kikwete. Pia katika kuonyesha mafanikio yake TAWLA watakuwa na maandamano ya amani kuanzia Mahakama ya H.akimu Mkazi Kisutu hadi Viwanja vya Mnazi mmoja. Pia kuzindua mkakati endelevu 2010-2014. Vilevile mnamo tarehe 10 Mei 2010 itatoa Msaada wa kisheria katika viwanja hivyo na kuendelea kwa wiki nzima kaunzia 11-14 Mei ,2010 kutoa huduma sehemu za Bagamoyo,Temeke(ofisi za UMATI)na TAWLA ofisi ya Ilala Shariffu Shamba jijini Dar es salaam, kulia ni Sakina Simba Mjumbe wa TAWLA.(Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)
Mwenyekiti wa (TAWLA) katikati Maria Kushonda Sakina Simba Kulia na Joaquiline De Mello mwanachama katika picha ya pamoja wakati wa mkutano huo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment