TAIFA STARS YABANWA MBAVU NYUMBANI NA VIJANA WA KAGAME AMAVUBI!!

Kocha wa timu ya Taifa Taifa Stars mbrazil Marcio Maximo akizungumza na waandishi wa habari jioni hii kwenye uwanja wa Taifa baada ya kumalizika kwa pambano la mpira wa miguu katika ya Taifa Stars na timu ya taifa ya Rwanda Amavubi uliopigwa jioni hii na Taifa Stars kulazimishwa sare ya magoli 1-1.

Katika mchezo wa leo taifa Stars ilizidiwa sana katika kiungo kwenye kipindi chote cha kwanza lakini mabadiliko yaliyofanyika kipindi cha pili kwa kumtoa Kigi Makasy na kumwingiza Mussa Hassan Mgosi yalizaa matunda kwa kuleta nguvu mpya iliyosababisha mshambuliaji Mrisho Ngasa kusawazisha goli baada ya Taifa Stars kufungwa dakika za mwanzo tu na mchezaji Roger Thous wa Rwanda.

Matokeo haya yanaipa wakati mgumu timu ya Taifa Stars wakati watakapokwenda Nchini Rwanda kurudiana na Amavubi katika jiji la Kigali, kwani inabidi washinde tu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele katika michuano hii ya komba la mataifa huru ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN kwani suluhu ya aina yoyote haitaisaidia chochote Taifa Stars.
Mshambuliaji wa timu ya Taifa Mrisho Ngassa akisikitika baada ya kukosa goli la pili kwa timu yake.
Marefa waliochezesha mpira wa leo wakiongoza timu za Taifa Stars na Rwanda wakati zilipokuwa zikiingia uwanjani tayari kwa mpambano wao leo kwenye uwanja wa Taifa.
Benchi la ufundi la Amavubi.
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars.
Kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda Amavubi

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment