
Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akisaini kitabu cha kumbukumbu mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la mpigania uhuru na Rais wa kwanza wa Uturuki hayati Mustafa kemal Pasha katika jengo la Historia ya kumbukumbu za kupigania Uhuru wa Uturuki Mjini Ankara Uturuki.

Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, akitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kama ishara ya kumkumbuka mpigania uhuru na rais wa kwanza wa Uturuki hayati Mustafa kemal Pasha katika jengo la Historia ya kumbukumbu za kupigania Uhuru wa Uturuki Mjini Ankara jana

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Spika ukitoa heshima za Mwisho

Spika akisindikizwa kuweka shada la maua

Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta, na ujumbe wa Bunge kutoka Tanzania wakiwa wamesimama kwa heshima kusikiliza wimbo wa Taifa la Uturuki mara baada ya kufika katika jengo la Historia ya kumbukumbu za kupigania Uhuru wa Uturuki.
0 comments:
Post a Comment