SHEREHE ZA MWENGE MKOANI MANYARA JANA!!

Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein akiwasha Mwenge Mkoani Manyara ,Wilaya ya Babati , (wa pili kushoto ) ni Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana Mhe. Juma Kapuya (Tanzania Bara) na ( wa pili kulia ) ni Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana (Zanzibar) Mhe. Asha Abdallah Juma akishuhudia uwashaji wa Mwenge huo jana.
( Picha zote na Anna Itenda _Maelezo)
Wazee wa Mji wa Babati Wakimtunuku silaha za jadi na mavazi ya jadi kuashiria kuwa anakaribishwa kuwa mwenyeji wao Mkoani Manyara ,wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mwenge jana.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara ndugu Hendry Shekifu(wa kwanza kushoto) akiimba wimbo wa Taifa akishirikiana na Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein wa pili kulia wakati wa uzinduzi wa Mwenge Mkoani Manyara Wilaya ya Babati jana.

Baadhi ya wananchi mbalimbali wa Mkoa wa Manyara Wilayani Babati wakiangalia na kushuhudia uzinduzi wa Mwenge Mkoani mwao jana
Chipukizi wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa Uzinduzi wa Mwenge Mkoani Manyara Wilaya ya Babati jana.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment