Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi tawi jipya la benki ya CRDB huko Marangu, moshi vijijini Jana mchana.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dr.Charles Kimei na kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Benki hiyo Martin Mmari.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo Aloyce Kimaro muda mfupi baada ya Rais Kikwete kufungua tawi jipya la benki ya CRDB katika kijiji cha Marangu,wilaya ya moshi vijijini.Kijiji cha Marangu ni sehemu ya jimbo la Vunjo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Vunjo Aloyce Kimaro muda mfupi baada ya Rais Kikwete kufungua tawi jipya la benki ya CRDB katika kijiji cha Marangu,wilaya ya moshi vijijini.Kijiji cha Marangu ni sehemu ya jimbo la Vunjo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia baadhi ya wananchi wa kijiji cha Marangu walihudhuria sherehe za ufunguzi wa tawi jipya la CRDB kijijini hapo jana mchana
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei muda mfupi baada ya kulifungua tawi jipya la Benki hiyo katika kijiji cha Marangu,wilaya ya moshi vijini jana mchana.Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo Bwana Martin Mmari
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro Lucas Ng'oboko akimuonesha Rais Jakaya kikwete chumba cha Mahabusu katika kituo kipya cha Polisi katika kijijicha Okaoni,Kobosho wilaya ya moshi vijijini jana muda mfupia baada ya Rais Kikwete kukifungua kituo hicho kilichojengwa kwa nguvu ya wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi nchini.Rais kikwete pia alifungua nyumba mbili mpya za maofisa wa polisi watakaotoa huduma katika kituo hicho.(picha na Freddy Maro)
0 comments:
Post a Comment