UONGOZI WA Chama Cha Mapinduzi (CCM),Wilaya
ya Kisarawe, umempongeza Kada wa chama
hicho, Maneno Mbegu kwa kitendo chake cha
kutangaza nia yake ya kutaka kugombea
ubunge wa Jimbo hilo kwa kutowapaka matope
viongozi waliopo madarakani.
ya Kisarawe, umempongeza Kada wa chama
hicho, Maneno Mbegu kwa kitendo chake cha
kutangaza nia yake ya kutaka kugombea
ubunge wa Jimbo hilo kwa kutowapaka matope
viongozi waliopo madarakani.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa CCM wa
Wilaya hiyo, Zena Mgaya mara baada ya Mbegu
kumaliza kuwatangazia wanaCCM, nia yake ya
kutaka kuwania nafasi hiyo, juzi katika
mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa CCM
Mjini Kisarawe. "Nimefurahi umejieleza vizuri, bila
kuwakashifu viongozi wengine,ndivyo
inavyotakiwa, na nakuomba hata huko mbele
ya safari uwe unafanya hivyo," alisema
Mgaya na kuwapa fursa wanachama kumuuliza
maswali Mbegu.
Mgaya, aliwaasa viongozi wa CCM, kuacha
tabia ya kwenda mitaani kuwapigia debe
waliotangaza nia ya kugombea, akidai kuwa
kufanya hivyo kunaweza kuwaharibia wao sifa
za uongozi pamoja na kuwawekea mazingira
magumu wagombea hao watakaopewa fursa
baadaye kujieleza kwa wanachama ambao
watawapigia kura na mmoja wao kufanikiwa
kuwa mgombea ubunge wa Jimbo hilo.Awali kabla ya kuanza kujieleza, Mbegu
ambaye hivi karibuni ameteuliwa na Mkuu wa
Mkoa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya
Sekondari ya Benjamini Mkapa, iliyopo
Jijijni Dar es Salaam,aliwashukuru viongozi
na wanachama waliohudhuria mkutano huo.
Mbegu, alisema kuwa elimu na uzoefu
alioupata kwa kutembelea nchi mbalimbali
duniani, atahakikisha anavitumia
kuliendeleza Jimbo hilo kwa ushirikiano na
wananchi.
"Nimezaliwa Kisarawe,nimesoma Kisarawe kwa
kutumia kodi zenu, hivyo sina budi kurejea
kuiendeleza Kisarawe,"alisema Mbegu na
kuongeza,
"Mimi ni miongoni mwa wanachama wanzilishi
wa CCM, 1977,Nimeamua kutangaza nia ya
kugombea ubunge wa Jimbo hili, kwa vile
najua kuwa ni haki yangu ya msingi ya
kuchagua na kuchaguliwa," alisema Mbegu.
Alisema kuwa wakati utakapofika atafafanua
zaidi ni namna gani atakavyoshirikiana na
wazee, wadogo zake na wananchi kwa ujumla
kuiendeleza Kisarawe.Mbunge wa Jimbo hilo
kwa hivi sasa ni Athuman Janguo
0 comments:
Post a Comment