NA JOSEPH ISHENGOMA-MAELEZO, Manyara
Makamu wa Rais Dr. Ali Mohamed Shein leo amezindua mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka huu (2010) katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati Mkoani Manyara.Ujumbe wa mbio za Mwenge mwaka huu umezingatia maeneo makuu mawili.
Eneo la kwanza ni mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria na UKIMWI chini ya kaulimbiu, “Maliza Malaria” na “Malaria haikubaliki.” “Zuia UKIMWI Timiza ahadi yako.” “Huduma za UKIMWI ni Haki za Binadamu kwa wote.” Na sehemu ya pili ay ujumbe wa mbio za Mwenge wa uhuru ni uchaguzi Mkuu mwaka 2010 chini ya Kaulimbiu, “Kumbuka hatima ya leo na kesho ya Watanzania imo mikononi mwako, jitokeze kupiga kura.”
Akihutubia wakati wa uzinduzi huo baada ya kusimikwa rasmi kuwa mzee wa Manyara, Makamu wa Rais amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ujao na kuwakataa wagombea wote watakao hamasisha vitendo vitakavyoashiria uvunjufu wa amani na utulivu wa Taifa.“Wale wote ambao watajihusisha na kuhamasisha chuki, utengano na ubinafsi miongoni mwa jamii, wakataeni kwani hawafai kuwa viongozi na watakuwa wamepungukiwa sifa za uongozi,’ amesema. “Kila mmoja ahakikishe anatumia haki yake ya msingi kushiriki katika ucahaguzi na kuzingatia sheria mpya ya fedha za uchaguzi na kujiepusha na mambo yote yaliyokatazwa katika sheria hiyo.
Kuhusu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, amekemea na kuwalaani watu wanaofanya mauaji hayo ambao amesema kuwa wana roho za kikatili na kutokuwa na imani na ubinadamu kwa ndugu zetu albino.“Wananchi mnaombwa kutoa ushirikiano wenu kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha na ukatili huu.
Serikali kwa upande wake itahakikisha vitendo vya ukatili na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi vinakomeshwa mara moja,”Mauajii ya watu wenye ulemavu wa ngozi yalianza nchini mwaka 2006 katika mikoa ya Shinyanga na Tabola na sasa yamekwisha samba nchi nzima ambapo jumla ya watu 40 wamekwisha uawa na wengine wanane wamejeruhiwa vibaya.
Aidha kuhusu ugonjwa wa Malaria, amesema ugonjwa huo unaoongoza kwa maudhurio ya wawagonjwa wanaofika kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya ambao ni kati ya asilimia 30 hadi 40 umekuwa mzigo mkubwa unaoelemea utoaji wa huduma za afya nchini.”Maudhurio hayo ni sawa na asilimia 30 hadi 40 ya maradhi mengine.
Kwa wastani ugonjwa huu wenye kinga umuua mtu mmoja kila dakika tano wengii wao wakiwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na Mama wanajwazito” amesema na kuongeza kuwa lengo la serikali ni kupunguza idadi hiyo ya vifo kwa asilimia 50 ifikapo 2013.Kuhusu madawa ya kulevya, Makamu wa Rais amewaagiza viongozi wa mikoa, manispaa, halmashauri za wilaya na taasisi mbalimbali kuhakikisha anakuwa na mipango endelevu ya ushirikishwaji na ushiriki wa wananchi wote katika kupambana na tatizo la madawa ya kulevya.“Matumizi ya daw za kulevya usababisha ukosefu wa huduma muhimu katika familia.
Na watumiaji wake hukosa busara za kutosha kufanya maamuzi juu ya namna ya kuilinda afya yake. Ili kuepuka tatizo hili., viongozi wa ngazi mbalimbali kuaanzia ngazi ya Taifa, mkoa, halmashauri na mashirika mbalimbali, lazima kuweka mipango mikakati na kuwashirikisha jamii katika mapambano haya.”Baada ya Makamu wa Rais kuzindua mbio hizo zilizoudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Kazi, Ajir ana Maendeleo ya Vijana Prof.
Juma Kapuya na WAziri wa Kazi, Vijana Maendeleo ya Wanawake na watoto Zanzibar Mhe. Asha Abdallah Juma, waakilishi wa mikoa ya Kagera, Kigoma, Mwanza, TAbora, Singida, Arusha, Kilimanjaro, Tabora Mara, Pwani na Shinyanga, Mwenge huo umekabishiwa kwa Mkuu wa mkoa wa Manyara Bw. Henry Shekifu ambaye pia amaukabidhi kwa uongozi wa wilaya ya Babati ambayo imekuwa ya kwanza mwaka hu kuukimbiza.
Mwenge huo unatarajiwa kumaliza mbio zake mkoani Manyara tarehe 2/6/2010 na kuendelea na mbio zake mkoani Arusha.
Kitaifa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu kinatarajiwa kuwa mkoani Kigoma Oktoba 14, 2010.
0 comments:
Post a Comment