Amesema yeye pamoja na mwenzake Barnaba wataweza kuwapa burudani ya aina yake mashabiki wa urembo wa jiji la Dar es salaam watakaohudhuria katika shindano hilo ambalo utakuwa ni uwakilishi wake wa kwanza wa kitongoji cha Dar Inter College kufanyika kwa mwaka huu baada ya kuundwa rasmi mwaka huu.
Jumla ya warembo 16 wanatarajiwa kuchuana katika shindano hilo linarotarajiwa kuwa la kuvutia kutokana na warembo watakaoshiriki kuwa katika viwango vya ushindani ambapo washindi watatu watakwenda kushiriki katika shindano la Miss Highlearning.
Warembo hao wananolewa na Miss Vodacom Tanzania namba mbili 2009 Beatrce Shelukindo huku Dansa wa siku nyingi Richard Yalomba aka "Bob Rich" akiwapa mazoezi makali ya kucheza kwa ajili ya Shoo ya ufunguzi kwa siku hiyo ya shindano.
Mratibu wa shindano hilo Silas Michel amewataja warembo wanaoshiriki katika shindano hilo kuwa ni Agness Francis, Sanza Mukajanga, Rosemary Muhoza, Pilly Hashim, Rahma Sway, Shone Mwanyanje, Basilisa Biseko, Catherine George, Rose John, Mary Lidya na Cassian Milinga.
Shindano hilo linadhaminiwa na RBP Oil & Industrial technology Ltd, Kmapuni ya bia TBL kupitia bia ya Redds Original Vodacom Tanzania, Shear Illusion, Michuziblog, Janejohn5blog, Fullshangweblog, Mtaa kwa Mtaablog, Condy Bureau Change na Dotnata Decorations
waliopo kwenye picha kutoka kushoto ni wanamuziki Amin, mratibu wa shindano Silas Michael na mwanamuziki Barnarba.





0 comments:
Post a Comment