Kwa ufafanuzi wangu utamaduni ni jumla ya mambo yote yanayobuniwa najamii husika ili kukidhi utashi na maendeleo yake ama ni mwenendo wamaisha ya kila siku ya jamii.Hapa kuna mtazamo wao wa mambo, taratibu zao za kuendesha maishaambazo zinawatofautisha wao na jamii nyingine.Utamaduni wa jamiihusika ndio kitambulisho kikuu cha taifa lolote na ni kielelezo chautashi na uhai wa watu wake.
Hivyo basi, tafsiri hii inaonyesha kuwa jinsi utamaduni unavyohusikana mchakato mzima wa maisha ya mwanadanu sambamba na maendeleo yakekiuchumi.Basi bwana, ili kuhakikisha kazi za sanaa na utamaduni unatoa mchangomuhimu na kuleta maendeleo serikali yetu inapaswa kuweka sheria nakanuni mazubuti katika maeneo ya ughramiaji , hadhi na kutoa fursa zamafunzo kwa wanautamaduni .
Hili likifanyika vema wanautamaduni watapiga hatua kutoka walipo nakufika juu zaidi katika sanaa , mikakati , mipango na itakuwa ni dirasambamba na kupunguza umasikini.Serikali inaweza kuondoa kodi katika vifaa vya kitamaduni na iachekuviona kuwa ni vya anasa na isimamie sheria ya hakishiriki nahatimiliki , pia inaweza kushirikiana na wasanii , mafundi katikauzalishaji kuwekeza katika utamaduni ama kudhamini.Aidha, serikali inao uwezo wa kuwapatia wanautamaduni wataalamu kutokanje ya nchi ili kutoa mafunzo ya teknolojia mpya kuhusu bidhaa ,masoko na jinsi ya kufanya utafiti kwenye tasnia hii.
Isitoshe wazalishaji na wasanii nao ni vema wakatambua kuwa wao niwashiriki wakuu kwenye eneo hili na wanaweza kupata kipato kikubwakuliko sasa na kuwa wanachangia uchumi wa taifa .
Inabidi pia waongezekuheshimu kazi zao katika kuzifanya kikamilifu , waoneze ubunifukatika kila kazi zao mpya na wahakikishe kazi zao mpya zinauzika.Tanzania Bara baada tu ya kufanikiwa kupata uhuru mwaka 1961, serikaliya Mwalimu Nyerere iliainisha matatizo makuu matatu ya wakati huo kuwani umasikini , ujinga na maradhi.
Tangu litoke tamko hilo serikali hile ilielekeza nguvu kwa namnambalimbali katika kupambana na matatizo hayo makuu matatu, huku ikitoamsisitizo kwa kubadilika badilika kadri muda ulivyokuwa unasogea.Ni vema sasa serikali ya awamu ya nne ikaipa aula tasnia ya utamaduniili kuwatoa wasanii wetu hapa walipo.Ni mimi Kimasa kutoka http://www.kingkif.blogspot.com/ unaweza kucheki namikwa kupitia simu : 0714-077040 ama email kingkif07@gmail .com.





0 comments:
Post a Comment