Watu 20 wanaswa kwa mauaji ya ushirikina!

Moja ya picha ikimwonyesha rais Ellen johnson sirleaf wa Liberia kushoto akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani na wakuu wa polisi Liberia.
Zaidi wa watu 20 wamekamatwa na polisi nchini Liberia, baada ya viungo vya mwili kupatikana katika makaazi ya afisa mmoja wa serikali.
Ripoti kutoka kusini mashariki mwa nchi hiyo zinasema, mama mmoja mjamzito aliuawa ili viungo vya mwili wake na kijusi kitumike kwa matambiko. Afisa mmoja wa serikali katika mji mkuu wa Monrovia ameiambia BBC kuwa habari hizo ni za kushangaza na kuhuzunisha na kuwa uchunguzi umeanzishwa.
Waandishi wa Habari wanasema eneo hilo limekuwa na historia ya mauaji ya ushirikina. Viungo vya mwili vinatumika kutengeneza hirizi za kujaribu kuimarisha ushawishi na madaraka ya kisiasa. www.bbcswahili.com

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment