WATANZANIA KUCHANGIA CHUO KIKUU (JOKUCO) KWA SMS!!

Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi kuu ya Magharibi, Elias Bubelwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa uchangiaji wa harambee kwa njia ya SMS Dar es salaam jana kwa ajili ya kuchangia uanzishwaji wa chuo kikuu cha Joshua Kibira university College(JOKUCO) mkoani Kagera
Na Mwandishi wetu
KANISA la Kilutheri Dayosisi ya Magharibi mjini Bukoba,limewataka watanzania kuchangia gharama za uanzishwaji wa chuo kikuu mjini humo kitakachofahamika kwama Joshua Kibira University College (JoKUCo). Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa kamati ya uwanzishwaji wa chuo hicho,Bw.Moses Kagya alisema chuo hicho kitagharimu sh.bilioni 1.3 ili kukamilika na kuanza kutumika.
Bw.Kagya alisema kuwa kuwa wananchi watachangia fedha kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) ambapo mchangiaji atatakiwa kutuma ujumbe wenye neno 'Mchango' na kutuma kwenda namba 15787. Alisema ujumbe huo utagharimu sh.350 ambapo namba za simu za wachangiaji zitaingizwa katika droo itakayochezwa kila alhamisi pale Mlimani City katika duka la The Game na washindi watazawadiwa zawadi mbalimbali.
Aliongeza kuwa Chuo hicho kinatarajiwa kuanza kuchukua wanafunzi wa mwaka wa kwanza Oktoba mwaka huu na kitafundisha masomo ya Ualimu,Biashara na Teknolojia (IT).

Mjumbe anayesimamia michango midogomidogo Bw. Charles Mwijage akimwonesha Televisheni aina ya LCD, itakayotolewa na kunadiwa wakati wa uchangiani wa harambee hiyo , Askofu Elias Bubelwa wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Magharibi jijini Dar es salaam jana.


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment