
Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Katibu Mtendaji wa tume ya Mipango na manaibu katibu watendaji wanne wa Tume hiyo.Katika hafla hiyo ilifanyika ikulu jijini Dar es Salaam .Rais amemwapisha Dr.Philip Isdor Mpango kuwa katibu Mtendaji wa tume hiyo na manaibu wake wanne akiwamo Bwana Maduka Paul Kessy, Bi.Happiness Mgalula, Bi.Florence Maridadi Mwanri na Bwana Klifford Katondo Tandari.Pichani (0076) Katibu Mtendaji wa tume hiyo Dr.Philip Mpango akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miongozo ya kazi Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Dr.Philip Isdor Mpango wakati wa sherehe za kumwapisha zilizofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.(picha na Freddy Maro)
0 comments:
Post a Comment