Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete amemteua Profesa Burton Lunogelo Mwamila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia kwa kipindi cha miaka mitatu.Aidha Waziri wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Technolojia Profesa Peter Msolla amewateua Bibi Joyce Mapunjo ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kuwa wajumbe wa Bodi hiyo.
Wajumbe wengine walioteuliwa ni pamoja na Profesa Mayunga Nkunya,Bwana Eliseta Kwayu ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwekezaji,Profesa Ester Mwaikambo kutoka Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Hurbert Kairuki.
Wengine ni Bi Christina Kilindu ambaye ni Katibu Mtendaji Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania,Profesa Evelyn Mbede ambaye ni Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia.Aidha wengine walioteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi hiyo ni Dokta Hassan Mshinda ambaye ni Mkurugenzi Mkuu ,Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia,Profesa Awadhi Mawenya ambaye ni Mshauri Mwelekezi kutoka Sekta binafsi.
Wajumbe Wengine walioteuliwa ni Bashiri Mrindoko ambaye ni Kamishna wa Nishati Wizara ya Nishati na Madini,Dokta Fidelis Myaka ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika.Pia uteuzi huo uliwajumuisha Dokta Abdulla Kanduru Mhadhiri kutoka Zanzibar State University na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii Dokta Felician Kilahama.Kabla ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia nchini Profesa Burton Lunogelo Mwamila alikuwa ni Makamu Mkuu wa Taasisi YA Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyopo Arusha Uteuzi huo wa miaka mitatu ulianzia tangu Tarehe 8 mwezi wa kumi na mbili mwaka 2009.






0 comments:
Post a Comment