Nigeria igawanywe pande mbili asema Gaddafi!!

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amesema Nigeria haina budi kugawanywa na kuwa mataifa mawili kuepuka umwagikaji zaidi wa damu baina ya Waislamu na Wakristo.
Akiwahutubia wanafunzi, amepongeza mfano wa India na Pakistan, ambapo kugawanywa nchi hizo kumeokoa maisha ya watu wengi.
Shirika la Habari la Libya, Jana likimkariri Kanali Gaddafi, akisema "Kuigawanya Nigeria, kutasaidia kukomesha umwagikaji wa damu na uchomaji majengo ya ibada."
Mwanadiplomasia mmoja mwandamizi wa Nigeria hakutilia maanani mapendekeo hayo ya Kanali Gaddafi.
Mamia ya watu wamekufa katika machafuko ya kidini vijijini sehemu mbalimbali za katikati ya Nigeria kwenye mji wa Jos mwaka huu.
Nigeria kwa kiasi kikubwa imegawanyika baina ya Waislamu upande wa kaskazini na Wakristo walio wengi kusini.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

2 comments:

  1. Duh, kumbe Ustaadh akitulia huwa ana mawazo mazuri sana. Sikutegemea kauli hii kutoka kwa bwana Ghadafi.

  2. Jamaa keshaanza mambo yake sasa, sijui huu mkutano wa waarabu utakaofanyika kwake utakuaje yani na ungoja kwa hamu sitaki kumiss, nione vichekesho na vipi atakavyowapakazia wenzake mtu huyu ni hatari ya danger yani, yetu mecho tu.

Post a Comment