NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
IMEELEZWA kwamba takribani watu bilioni 1.1 duniani kote wamatumia maji yasiyo salama huku wengine bilioni 2.5 hawana huduma ya usafi wa mazingira yaani uondoaji wa maji machafu na vyoo.Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Christopher Chiza kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa(UN), wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu wiki ya maji. Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya wiki hiyo ambayo inaanza rasmi leo(kesho) yatafunguliwa na Naibu Waziri Chiza, hadi 22, Machi mwaka huu. Maadhimisho hayo yanafanyika mkoani Pwani, wilaya ya Kibaha, uwanja wa Mwendapole ambapo shughuli mbalimbali zitafanyika.Mgeni rasmi katika siku ya kilele anatarajiwa kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha. Kauli mbinu ya maadhimishoa ya wiki hiyo inasema ‘Maji Safi na Salama kwa Afya Bora, ambayo inasisitiza umuhimu wa ubora wa maji. Aidha Waziri Chiza aliongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya UN, karibu watoto milioni 1.5 hufariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa yanayotokana na ukosefu wa huduma hizo.Naibu Waziri huyo alisema taarifa hiyo ya UN, inaeleza kwamba karibu tani milioni mbili za maji taka yanayozalishwa duniani na kumwagwa kwenye maji ya mito, maziwa na bahari, lakini hayatumiwi katika kilimo cha umwagiliaji.Hivyo asilimia 80 ya majitaka katika nchi zinazoendelea huachwa ya kitapakaa ovyo kwa sababu ya ukosefu wa miundombinu ya kuyadhibiti. Wakati huohuo Waziri Chiza alizungumzia kuhusu tatizo la upatikanaji wa majisafi na salama katika jiji la Dar es Salaam, ambapo asilimi 68 ndio wanaopata huduma hiyo ikilinganishwa asilimia 84 katika miji mingine alisema juhudi mbalimbali zinafanyika ili kuweza kulitatua.Alisema wizara yake inaendelea kurabati vituo na mitambo ya kuzalisha maji na kutafuta vyanzo vingine vya maji viwemo vya maji chini ardhi, na kujenga bwawa Idunda.Waziri Chiza alifafanua kuwa mahitaji ya maji katika jiji hilo ni meta za ujazo 470,000 ,wakati uzalishaji ni meta za ujazo 270,000. Kwa upande wa vijiji asilimia 63 ndio wanaopata maji hayo kwa sasa.Alisema kupitia Mpango wa Taifa wa Kukuza Uchumi(MKUKUTA) ifikapo mwaka 2010. Asilimia 90 ya watu miji wawe wanapata maji safi na salama, huku asilimia 65 kwa upande wa vijijini.





0 comments:
Post a Comment