MULTCHOICE YAZINDUA KITUO CHA KURUSHA VIPINDI VYA DSTV SHULE YA SEKONDARI JANGWANI!!

Kaimu katibu mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Selestin Gesimba kulia, Meneja Mkuu wa Multchoice kushoto na Kaimu mkuu wa shule ya Sekondari Jangwani Mrs Ruteganya wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha kurushia vipindi mbalimbali vya DSTV kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi shuleni hapo tayari Multchoice imeshaanzisha vituo kama hivyo katika mikoa ya Morogoro Mbeya Iringa Arusha na mingine.
Lengo la Multichoice ina lengo la kufungua vituo hivyo zaidi ya miamoja katika kipindi cha miaka mitano ijayo ili wanafunzi zaidi waweze kupata nafasi ya kutumia huduma hiyo katika shule zao.
Wanafunzi wakiwa wamepozi katika picha mara baada ya king'amuzi hicho kuzinduliwa rasmi leo.

Mwanafunzi Catherin D. Mlay wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Jangwani akiwa ameshikilia chombo kilichohifadhi mkasi kwa ajili ya kukatia utepe katika uzinduzi wa kituo cha kurushia vipindi vya DSTV, kituo kimezinduliwa na kaimu katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi Selestin Gesimba.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Jangwani wakiimba wimbo maalum mbele ya wageni wakati wa uzinduzi wa king'amuzi cha kurushia vipindi mbalimbali ya DSTV yanayotoa elimu ya mambo mbalimbali kwa wanafunzi, king'amuzi hicho kimefungwa na kampuni ya Multchoice.
Meneja Masoko wa Multchoice Tanzania Furaha Samalu kushoto akiongea na Meneja uhusiano wa kampuni hiyo Barbara Kambongi.
Meneja mkuu wa Multchoice Tanzania Peter Fauel kulia akijadiliana jambo na watendaji wake Furaha Samalu Meneja Masoko na Barbara Kambongi Meneja uhusiano wakati wa uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya DSTV katika shule ya sekondari ya Jangwani leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment