MTEJA WA ZANTEL ACHOMOKA NA VESPA ZANZIBAR!!


Zantel leo imeendesha droo yake ya kwanza ya promosheni ya CHOMOKA NA VESPA ambapo Bw. Mkombe Juma Khamis mwenye umri wa miaka 45 ambaye ni mkulima mkazi wa Upenja visiwani Unguja amebahitika kujishindia pikipiki aina ya Vespa.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa droo hiyo iliyohudhuriwa na wakazi wengi wa Zanzibar Meneja masoko wa kampuni ya Zantel Bw. William Mpinga alimpongeza Bw. Mkombe kwa kuwa mteja wa kwanza kujishindia Vespa hiyo.
Naye Bw.Mkombe ameelezea furaha yake baada ya kupata habari za ushindi wake kwa njia ya simu na kusema kuwa Vespa hiyo itamsaidia sana katika shughuli zake za kila siku kwani sasa amepata chombo cha usafiri.
“Hii ni droo ya kwanza ya promosheni Chomoka na Vespa kwa
hiyo bado kuna muda wa wiki 7 na droo 7 zilizobakia na zawadi ambazo bado zinashindaniwa ni pamoja na Vespa 7, Baiskeli 21, Simu za mkononi 21 na vocha 35 za muda wa maongezi wa Tsh 10,000. Zawadi hizi zitaendelea kutolewa kila wiki ambapo tutakuwa tukitoa Vespa 1 kila wiki, baiskeli za kisasa 3, simu za mkononi zinazotumia mwanga wa jua 3 na vocha 5 za muda wa maongezi wa Tsh 10,000 kila wiki kwa muda wa wiki 7 zilizobakia,” alisema Bw. William
Washindi wengine katika droo ya promosheni hiyo ni pamoja na Bw Juma Hamisi Juma, Bi. Riziki Aimer na Bw Said Salum ambao wamejishindie zawadi za baiskeli za kisasa kila mmoja. Bw Rashid Salum, Bw Makame Bakari Na Bw Kassim Ali Ahmada ambao wamejishindia simu za mkononi zinatumia nishati ya jua kila mmoja na Bw Abdullah Mohd, Bw. Abdulla Mtumwa, Bw Ibrahim Juma Mohamed na Bw. Hamad Suleiman ambao wamejishindia muda wa maongezi wa Tsh 10,000 kila mmoja.
Meneja huyo ameendelea kusema kwamba washindi wote wanatakiwa kufika makao makuu ya Zantel Zanzibar ili kuchukua zawadi zao.
Ili kushiriki katika promosheni hiyo mteja wa Zantel atatakiwa kuweka muda wa maongezi wa Tsh 1,000 au zaidi na kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno VESPA kwenda namba 15583. Ujumbe huo utatozwa Tsh 350 pamoja na VAT. Mteja anaweza kutuma SMS nyingi kadri awezavyo ili kujiongezea nafasi za kushinda.
Droo za promosheni hii zitafanyika kila Jumatatu ambapo washindi watapigiwa simu na kutaarifiwa kuhusu ushindi wao na hatimaye kupewa zawadi zao.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment