Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa wateja wa Shirika la Bima la Taifa 2010 Ltd Bw. Aloyce Mwasuka akizungumza na mawakala wa shirika hilo nchini wakati wa kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa makao makuu ya shirika hilo mtaa wa samora jijini Dar es salaam, kikao hicho kilikuwa ni mpango maalum na mzuri kwa ajili ya kufahamiana kati ya mkurugenzi huyo wa masoko na mawakala wake, na kwa kuwa ni mgeni alipenda kukutana nao na kupanga mikakati mipya na mizuri kwa ajili ya kuboresha zaidi huduma za shirika na kupeana changamoto za kihuduma ili kuanza upya na kuangalia mbele nini kifanyike kwa kuangalia shirika lilikotoka, lilipo na linakokwenda, lakini pia ilikuwa kuelimishana kuhusu utoaji wa huduma kwa wateja ili kuboresha zaidi na zaidi huduma za shirika hilo mama la bima nchini.Miongoni mwa kampuni za mawakala zilizoshiriki katika kikao hicho ni Barak Insurance Agency, Mchome Insurance Brokers, Msambo Agency,Antony Mathew Masala, A.A Mcheka Agency, Tonni Masaburi Aneto Insurance, MwakasangaLife HSE Agency,Nafue Abdalla Agency, Zakaria Mbulu Agency, Henrod Makule Agency na nyingine.
Shirika hilo kwa sasa linafanya mikakati mingi ili kuboresha huduma zake hivyo kujenga misingi bora na imara ya kibiashara kwa wateja wake.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakisikiliza maoni mbalimbali yaliyotolewa na wajumbe.
Wajumbe mbalimbali wakimsikiliza mkurugenzi wa masoko na huduma kwa wateja wa shirika hilo Bw Aloyce Mwasuka hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza nao katika mkutano uliofanyika leo jioni makao makuu ya shirika hilo




0 comments:
Post a Comment