Meli ya Saudia yatekwa Ghuba ya Aden!

Moja ya meli ya Kisaudia ikiwa katika safari zake.

Maharamia wa Kisomali wameiteka nyara meli kubwa ya Saudia katika Ghuba ya Aden.
Meli hiyo Al Nisr Al Saudi, ilikuwa na mabaharia 14 lakini haikubeba mafuta.
Nahodha wa meli hiyo ni raia wa Ugiriki ma mabaharia wengine wanaamika ni raia wa Sri Lanka.
Kwa mujibu wa wanajeshi wa majini wa mataifa ya Ulaya wanaopiga doria katika eneo hilo, maharamai wa Kisomali wanashikilia meli sita na mabaharia 132.
Matukio ya utekaji meli katika Ghuba ya Aden huongezeka katika miezi ya Machi , Aprili na Mei kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment