BBC imepata ushahidi wa mauaji ya hivi karibuni ya zaidi ya watu 300 katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Mauaji hayo yamefanywa na waasi wa kundi la LRA, ambao walivamia vijiji kadhaa kwa muda wa siku tano mwezi Disemba mwaka jana.
Mwandishi wa BBC ambaye ametembelea eneo la kaskazini mashariki mwa Kongo amesema waasi, walivamia nyumba za watu, kufanya uporaji, kubaka na kuua watu kwa mapanga na marungu.
Kundi la LRA liliundwa zaidi ya miaka 20 iliyopita nchini Uganda, lakini hivi sasa linafanya shughuli zake katika maeneo ya kaskazini mwa Kongo, kusini mwa Sudan na katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kundi la wanaharakati wa haki za binaadam la Human Rights Watch ambalo limetoa taarifa hizo za mauaji limesema ni muhimu Umoja wa Mataifa kuongeza wanajeshi zaidi nchini Kongo. http://www.bbcswahili.com/

0 comments:
Post a Comment