MAMBO YA TWANGA VIWANJA VYA LEADERS JANA JIONI!!

Wanenguaji wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) wakizungusha viuno vyao katika onyesho lao lililofanyika kwenye Bonanza la jumapili pale viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam, katika onyesho hilo pia kundi la walemavu la Tunaweza Band lilifanya mambo yake na kuwavutia mashabiki wengi kutokana na kupiga muziki wa kiasili.
Mkurugenzi wa African Stars Asha Baraka akizungumza na mwana CCM mwenzie Abas Masoud ambaye ni katibu mwenezi kutoka tawi la Vigaeni Magomeni, haikuweza kufahamika walikuwa wakijaili nini, hata hivyo Asha Baraka ameonyesha nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM japokuwa hajasema kuwa atagombea katika jimbo gani.
Fredie Fredito kushoto mdau mkubwa wa Twanga akipiga story na wadau wenzake jana wakati wa bonanza lililofanyika katika viwanja vya Leaders.
Vimwana wa Bendi ya African Stars wakipozi kwa picha kabla ya kupanda jukwaani katika onyesho lao jana bendi hiyo hufanya onyesho kila jumapili kwenye bonanza la Leaders jijini Dar es salaam.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. mbona mvuto sijauona yuko wapi aisha madinda .....hapo hakuna mvuto zaidi ya queen suzi

Post a Comment