NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Christopher Sayi amesema kwamba utumiaji wa Tekonoljia ya Habari na Mawasiliano(TEKNOHAMA) ni nyezo madhubuti katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya ndani na nje ya nchi.Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu huyo wakati akifungua mkutano wa siku moja wa uandaaji wa rasimu ya mkakati wa TEKNOHAMA wa wizara hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi na Sera na Mipango Damas Shirima.“TEKNOHAMA inahusisha maisha ya watu,namna watu wafanyavyo kazi na jinsi taasisi zinavyofanya kazi. Kwa manitiki hiyo ina mchango katika uchumi mkubwa na mdogo,” alisema Sayi.
Alisema TEKNOHAMA inawezesha maendeleo ya kijamii na kuchumi, lakini changamoto inayoikabili nchi yetu utumiaji wake katika masuala ya kiuchumi na manufaa ya Watanzania.Hivyo watunga sera wanatakiwa kuhakikisha kuwa Sera ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mwasiliano inaenda sambamba na kutekeleza Sera za Taifa za Uchumi.Akizungumzia kuhusu umuhimu wa TEKNOHAMA katika wizara yake, inayotarajiwa kuanza kutumika mwaka ujao wa fedha, alisema itasaidia kutekeleza Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji(WSDP) na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo(ASDP) hususan kwenye usimamizi wa twakimu na mawasiliano ya kati ya wizara na wadau wake.
Naye Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Mkuu ,kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma., Frank Shame ambaye alikuwa mwezeshaji wa rasimu hiyo alisema uhaba wa wataalamu kwenye eneo hilo, ni changamoto inayoikabili Serikali katika kutekeleza mfumo huo. Shame alisema uelewa mdogo wa dhana ya TEKNOHAMA kwa baadhi ya wadau, (kwa matumizi ya serikali inajulikana kwa jina Serikali Mtandao), wananchi bado hawana mwamko mkubwa na imani katika kutumia mifumo hii.Alizitaja changamoto nyingine kuwa ni uhaba wa fedha katika kuibua na kutekeleza miradi mbalimbali ya Serikali Mtandao na uwezo mdogo wa kifedha kwa wananchi walio wengi hali inayosababisha kushindwa kushiriki kikamilifu fursa zipatikanazo kupitia Serikali Mtandao.
Alisema ukosefu wa miundombinu ya mawasiliano ya kompyuta kwa ajili ya kuunganisha ofisi zote za Serikali mfano vijijini.Mkutano huo ulihusuisha wadau mbalimbali kutoka, wizara hiyo vyuo vikuu, Idara za Serikali na wafadhili.
0 comments:
Post a Comment