Wachezaji wa Timu ya Simba wakishangilia mara baada ya kupata goli la kwanza ililofungwa na mchezaji Mussa Hasaa Mgosi katika kipindi cha kwanza cha mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya timu hiyo na JKT Ruvu iliyopigwa leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.Mchezo huo ulikuwa ni mgumu sana hasa kwa timu ya Simba kwani ilikuwa ikihitaji pointi tatu muhimu kutoka kwa timu ya JKT Ruvu ili iweze kujihakikishia ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2010/2011 ugumu huo ulipelekea wachezaji wa Simba kupigana kufa na kupona ili kuhakikisha wanaondoka na ushindi katika siku ya leo.
Katika kipindi cha pili dakika mbili za mwisho zilitosha kabisa kuifanya Simba iibuke na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya JKT Ruvu iliyokuwa ikibana vya kutosha kuhakikisha kwamba angalau na yenyewe iondoke uwanjani ikiambuli suluhu.
Lakini alikuwa Mgosi tena na mchezaji aliyetokea benchi Uhuru seleman walioizamisha kabisa manuwari ya JKT Ruvu wakati walipofunga goli mbili zingine za haraka zilizofanya Simba kuondoka na ushindi mnono wa magoli tatu na pointi tatu dhidi ya JKT Ruvu kutoka mkoa wa pwani goli la JKT lilipatikana kwa njia ya penati katika kipindi cha kwanza.
Simba imefikisha pointi 53 katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom iukifuatiwa kwa mbali na Yanga yenye point 42 kama timu hiyo itashinda leo wakati itakapopepetana na Timu ya Azam Fc itafikisha pionyi 45 na kuwa na tofauti ya pointi 10 kati yake na Simba inayoogoza ligi hiyo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia na watoto kwa staili ya Umefulia
Golikipa wa JKT Ruvu akiruka juu kuokoa mpira
Mwamuzi Israel Nkongo akimuonyesha kadi nyekundu mmoja wa wachezaji wa JKT Ruvu aliyefanya mazambi
Golikipa wa JKT Ruvu Juma Dihile akitolewa nje baada ya kuumia wakati alipogongana na Mussa Hassan Mgosi katika purukushani za kuokoa mpira






2 comments:
haluuu yanga mmefuria
KUMBE HAWA JAMAA WOOTE SIMBA, DUHH.. NDIO MAANA TUNAONA COMMENT ZAO NI ZA KINAZI SIKU ZOTE!!!!
Post a Comment