WAZIRI MWANDOSYA AKAGUA MIRADI YA MAJI KIBAHA!!

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya (kulia) akiwatambulisha maafisa wajenzi wa mradi huo wa maji wa kampuni ya CHINA ANNENG CONSTRUCTION CORP. (CCACC) jana kwa wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika ofisi ya Halmashauri Wilaya ya Kibaha kata ya Soga.Pichani alivaa kofia ni CAO Yang .na mwengine ni WANG FEI.
Picha na Mwanakombo Jumaa wa MAELEZO.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya na Mbunge wa Kibaha Vijijini Ibrahim Msabaha wakimsikiliza mkazi wa Kibaha Vijijini alipokuwa akitoa maelezo jana wakati Waziri Prof. Mwandosya alipofanya ziara ya kutembelea Miradi ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Soga -Kibaha ambapo pia alitembelea shule ya sekondari ya Rafsanjani na kuongea na wanafunzi wa shule hiyo wanafunzi hao walimsomea risala yao kuhusu kero ya maji shuleni hapo.
Baaadhi ya watoto waliokuwa wakisubiri maji kwa muda mrefu huko soga msikitini jana wakifurahi maji baaada ya mradi uliopo sasa unaotandika mabomba wa kampuni ya CHINA ANNENG CONSTRUCTION CORP.(CCACC) kufikisha zoezi la utandikaji wa mabomba kijiji hapo hivyo wanakiji kuweza kupata huduma maji .

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment