Mwanasheria wa kujitegemea Bw. Deiniol J. Msemwa akitangaza nia yake ya kugombea ubunge jimbo la Njombe Kusini Mkoani Iringa kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi wa Rais na Wabunge unaotarajiwa kufanyika baadae mwezi Oktoba mwaka huu endapo atapitishwa na chama chake.
Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo na yeye mwenyewe akapata wasaa wa kuongea na wanahabari na kuwatangazia nia yake hiyo.
Jimbo hilo kwa sasa linashikiliwa na Mwanasiasa Mkongwe ndani ya CCM mwanamama shupavu Anna Makinda ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dainiol Msemwa amesema ametuhubutu kutangaza nia yake hiyo kwa kuwa uwezo anao na katiba ya chama cha mapinduzi inamruhusu kufanya hivyo, lakini pia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa haki hiyo ya kuchagua ama kuchagulia kama raia wa Tanzania.
Katika Picha wengine wanaofuatia ni Enock Ngombale Mwiru Mshauri wa siasa wa mgombea na mwisho ni Jerome Joseph Msemwa wakili.
0 comments:
Post a Comment