Wachezaji wa Chelsea wameelezwa tabia mbaya hazitavumiliwa kufuatia kuondolewa unahodha wa England John Terry kutokana na kuwa na uhusiano nje ya ndoa.Baada ya mkutano mfupi uliohudhuriwa pia na Mtendaji Mkuu wa klabu Ron Gourlay, meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti amesema kulinda hadhi ya klabu ni jambo muhimu zaidi.
Ameendelea kusema, sasa wanaelewa nini cha kufanya na ni tabia ya aina gani inayokubaliwa wanapokuwa wamevaa fulana ya Chelsea.
Mlinzi wa kushoto wa Chelsea Ashley Cole naye pia ametumbukia katika dimwi la kukiuka ndoa yake.
Viongozi hao Ligi Kuu ya Soka ya England, wamekuwa kwa wiki kadha wakitajwa katika vyombo vya habari kuhusiana na vitendo vya baadhi ya wachezaji wako.





0 comments:
Post a Comment