UNENE WAMKOSESHA SAFARI KELVIN SMITH!

Muongozaji na mchezaji wa filamu wa huko Marekani, anayekwenda kwa jina la Kevin Smith, alijikuta akiwa katika vita kubwa ya maneno na shirika la ndege la Southwest la huko Marekani kuanzia siku ya Jumapili hadi Jumatatu nzima kupitia mtandao wa Twitter.
Ugomvi huo wa maneno ulianza pale Southwest walipomnyima Smith kusafiri na ndege yao kwa kile walichosema jamaa huyo ni mnene mno kutosha katika viti vya ndege hiyo.
Smith baada ya kuzodolewa na ndege hiyo akazama ndani ya ukurasa wake wa Twitter na kuwatupia kijembe kwa kusema, "You have messed with the wrong sedentary, processed-foods eater," (Mmeingia choo cha kike kwa kuanzisha ligi na mpenda vyakula vya makopo) - Tasfsiri ni ya kwangu.Smith ambaye ni maarufu kwa kuongoza filamu ya "Clerks" anasema alijaribu kuchukua usafiri wa Southwest siku ya Jumapili lakini akapigwa chini japo aliwadhirihishia kwamba anatosha kwenye kiti cha ndege hiyo na pia anaweza kufunga mkanda bila ya shida yeyote.
Smith ambaye amekuwa haonei aibu umbo lake kubwa amesema mara zote huwa akinunua siti mbili katika ndege kwa safari zake, na alifanya hivyo kwa usafiri wa Jumapili iliyopita pia, lakini kosa alilofanya ni kwamba alichukuau ndege iliyokuwa ikiondoka masaa kadhaa baadae wakati yeye alitaka kufika anakokwenda mapema, hivyo akaingia kwenye ndege nyingine ambayo ilikuwa na siti moja tu iliyo wazi.
Alipoingia kwenye ndege hiyo rubani akamwambia hawezi kusafiri humo kwa sababu hatoshi kwenye hiyo siti iliyokuwa imebaki na asubiri ndege inayofuata.
Lakini katika blogu posti aliyotuma Jumapili, Smith anasisitiza, "Nilikuwa natosha bila shida kwenye siti ile...na niliweza kufunga mkanda bila tatizo lolote...hata hivyo wakanibania".Southwest wakamjibu kupitia blogu yao kwamba, "Ukweli ni kwamba Smith alielekezwa na wahudumu wetu kwa nini tulifikia uamuzi ule, na tulimpatia vocha ya dola 100 kwa usumbufu uliotoke na kwamba alikuwa akiandaliwa usafiri mwingine katika ndege inayofuata."Hata hivyo Smith ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni moja katika mtandao wa Twitter akawajibu tena Southwest akisema kwamba jamaa badala ya kumuomba radhi wanaendelea kumnyanyapaa katika blogu posti yao.Habari kutoka http://fotobaraza.ning.com/profiles/blogs/unene-wamponza-kevin-smith

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment