Bi.Eliza Michael ambaye ni mlemavu wa ukoma anayeishi kwenye makazi ya watu wenye ulemavu cha Nazareti,wilayani Kilombero akishona mkeka kwa ajili ya kujipatia kipato.
Na. Catherine Sungura,MOHSW
Jamii nchini wametakiwa kuachana na imani potofu zinazohusisha ugonjwa wa ukoma ni wa kuroga,laana au dhambi.
Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki kwenye hotuba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kanali Mstaafu Issa Machibya kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya ukoma duniani iliyofanyika wilayani Kilombero.
Machibya alisema kutokana na imani potofu watu walioathirika na ukoma wamekuwa wakitengwa katika jamii na hivyo kuogopwa sana hasa kutokana na kusababisha ulemavu.
Alisema licha ya historia ya ukoma kuwa ni ya enzi karne , kuna tofauti kubwa iliyopo sasa na enzi hizo, ambapo sasa kuna dawa zinazotibu kwa ukamilifu ugonjwa huo.
“Ukoma unatibika na tunazo dawa za kutosheleza, dawa hizi zinatolewa bila malipo katika vituo vyote vya tiba vya serikali, mashirika ya dini na mashirika binafsi”.
Aidha aliwataka wananchi hasa katika maeneo yanayoendelea kuripoti wagonjwa wengi kuhamasisha wananchi na kutambua dalili za ukoma na kupata tiba mapema.
Aliongeza kuwa tiba ya ukoma inachukua kati ya miezi sita hadi mwaka kulingana na aina ya ukoma, hivyo mgonjwa aliyeanza tiba hawezi kuambukiza mtu mwingine na hivyo hakuna sababu ya kuwa na hofu au kumtenga mgonjwa kwani anaweza kuendelea na shughuli zake za kawaida za maisha ya kila siku.
Mapema Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando alisema takwimu za nusu mwaka za 2009 zinaonyesha kuwa ukoma unaendelea kupungua nchini ukilinnganisha na mwak 2008 ambapo jumla ya wagonjwa 1,281 waligundulika na ugonjwa huo hiyo ni pungufu kwa asilimia 25.
Alisema takwimu za mwaka 2008 jumla ya wagonjwa 3,437 wa ukoma waligundulika, kati ya hao 3,250 sawa na asilimia 94.5 walikuwa wagonjwa wapya na 189 sawa na asilimia 5.5 walikuwa wamerudiwa tena ugonjwa.
“Mwaka 2006 Tanzania ilifikia lengo la kimataifa la kutokomeza ukoma kitaifa, yaani idadi ya chini ya mgonjwa mmoja kwa kila watu 10,000, aidha pamoja na mafanikio hayo bado kuna mikoa haijafikia lengo hilo”.Alisema Dkt. Mmbando
Alitaja mikoa ambayo haikufikia lengo hilo ni Lindi (2.3), Rukwa (2.0), Tabora (1.6), Morogoro (1.5), Mtwara (1.3) na Dare es Salaam (1.2).
Hatahivyo alisema Wizara inaendelea kufanya kila liwezekanalo ili mikoa ifikie lengo la kimataifa kwa kupanga mikakati ya kuhamasisha wananchi juu ya dalili za awali za ukoma pamoja na kuhakikisha uongozi ngazi ya kata .tarafa na wilaya wanaelewa vizuri lengo hilo la kutokomeza ukoma.
Aidha aliitaja mikoa yenye wagonjwa wngi nchi ni pamoja na Mwanza 372, Rukwa 336, Dar es Salaam 331, Morogoro 330, Kagera 298, Lindi 201, Tanga 191, na Kigoma 175.

0 comments:
Post a Comment