Kundi la Sweat Noise huwa linafanya maonyesho yake kila siku za Jumatano na Jumapili Club VIP, Ijumaa na Jumamosi Luxury Pub.
Bendi hii ilianzishwa kwa lengo la kuwaburudisha wakazi wa Manispaa ya Iringa ambao kwa muda mrefu sasa walikosa burudani ya muziki wa Dansi kwa kila wikiendi.
Mara nyingi walikuwa wakitegemea Bendi za Dar es salaam ambazo zilikuwa zikitoza kiingilio kikubwa sana na hivyo kupelekea baadhi ya mashabiki kushindwa kumudu gharama za viingilio.
Bendi hiyo inawakaribisha katika maonyesho yao mashabiki na wapenzi wa muziki wa mkoani Iringa na vitongoji vyake pamoja na wageni mbalimbali wanaotembelea mkoani humo kwani hawatajuta kwenda kuiona bendi hiyo bali watafurahia burudani hiyo.





0 comments:
Post a Comment