Aliyekuwa mwenyekiti wa Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma na mjumbe wa NEC wa Chama cha siasa cha CHADEMA Bw. Felix Mkosamali akitangaza rasmi uamuzi wake wa kujitoka katika chama hicho na kujivua uanachama wakati alipoongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo asubuhi.Mkosamali amesema chama cha CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na katibu wake Wilbroad Slaa nimejiridhisha kwamba yale yaliyonifanya niichukie CCM ndiyo yanayoendelea CHADEMA chini ya Freeman Mbowe.
Ameongeza kuwa Chama hicho pia kinaendeshwa kikabila kwani mtandao mzima wa fedha wa CHADEMA unashikiliwa na wachaga ameongeza kuwa kwa sasa ataendelea kuwa mwanaharakati wa kisiasa lakini bado hajaamua ajiunge na chama gani cha siasa, lakini wakati utakapofika atatangaza rasmi, aliyeko kushoto katika picha ni Afisa habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Mwirabi Sise.





0 comments:
Post a Comment