Jumuiya ya Wachina nchini yaisaidai WAMA!

Benjamin Sawe
Maelezo Dar es Salaam
Jumuiya ya watu wa China wanaoishi nchini jana imekabidhi jumla ya kiasi cha dola za kimarekani 113,330 ikiwa ni msaada wa dawa za kupambana na ugonjwa wa malaria pamoja na hundi ya seti za majiko ya kutumia umeme wa jua.
Makabidhiano hayo yamefenyika jana katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa kichina ambapo Mama Salma aliushukuru Ubalozi wa China pamoja na jamii ya wafanyabiashara wa Kichina kwa misaada mbalimbali kwa taasisi ya wanawake na Maendeleo Tanzania WAMA.Mama Salma alisema wataalamu wa kichina wamekuwa wakitoa huduma katika maeneo ya afya,elimu na miundombinu hivyo kuleta chachu katika maendeleo ya jamii bali kuongeza ushirikiano kati ya China na Tanzania.Alisema kukaa pamoja baina ya watu kutoka mila na damaduni mbalimbali vimesaidia kujenga msingi wa amani katika nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuvutia shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazohusisha mila mbalimbali.“Umuhimu wa kufanyika sherehe hizi hapa Tanzania unatokana na ongezeko la idadi ya Wachina wanaoishi hapa nchini pamoja na kuimarika kwa uhusiano baina ya nchi zetu mbili.Alisema mama Salma.Akizungumzia kuhusu mdororo wa uchumi ambao uliathiri maeneo ya biashara,utalii,mapato ya serikali na ukuaji wa uchumi mama Salma alimshukuru Mungu kwa kuvuka kipindi hicho kigumuMama Salma aliongeza kuwa hali hiyo ya kunusuru uchumi imetokana na mpango wa Tanzania wa kuunusuru uchumi pamoja na ushirikiano mzuri wa jamii ya kichina na jumuiya ya kimataifa.Nae Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng alisema licha ya mdororo wa uchumi duniani lakini uhusiano wa China na Tanzania umeendelea kuimarika na ameahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali.Balozi Liu Xinsheng alifafanua kuwa kufanyika kwa sherehe za mwaka mpya wa Kichina nchini ni ishara ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi ya Tanzania na China.Hii ni mara ya kwanza kufanyika kwa sherehe hizi za mwaka mpya wa kichina hapa nchini ambazo ni kongwe na muhimu kuliko sherehe zote katika kalenda ya Kichina.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment