JUMLA YA MILIONI 22 ZATENGWA KWA ZAWADI KILIMANJARO MARATHON!

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui (shati la mistari) akifafanua masuala mbalimbali kwa wandishi wa habari jijini leo kuhusu mbio za nyika za 2010 ambazo zitafanyika mwisho wa mwezi wa Februari 2010 mkoani Kilimanjaro. mwigine ni Meneja ya Bia ya Kilimanjaro George Kavishe.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania(RT) Suleiman Nyambui (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini leo kuhusu wakimbiaji wa mbio za nyika za Kilimanjaro 2010 ambazo zitafanyika mwisho wa mwezi huu Mkoani Kilimanjaro(kulia) ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe.. (Picha na Mwanakombo Jumaa.-Maelezo)

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema kuwa “zawadi za washindi wa mbio ya kilomita 42 kwa wanawake na wanaume ni shilingi milioni 7.5 na jumla itakuwa ni shilingi milioni 15.
Washindi wa mbio za kilomita 42.2 kwa wanaume na wanawake watajipatia shilingi milioni 3 kila mmoja, washindi wa pili watajipatia shilingi milioni 1.5 kila mmoja na washindi wa tatu watajipatia shilingi 850,000 kila mmoja. Washindi wa kilomita (nusu marathon) watajishindia shilingi milioni 1.5, washindi wa pili watajipatia shilingi 750,000 na washindi wa tatu watajipatia shilingi 425,000 kila mmoja.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kutangaza zawadi jijini Dar es salaam leo, Kavishe alisema kuwa lengo la kuendelea kutoa zawadi za kuvutia ni kutokana na ukweli kwamba dunia nzima wanariadha wanalipwa vizuri.
“Tunaishi kwenye dunia ambayo wanariadha wa mbio ndefu wanastahili kulipwa vizuri, kama ilivyo kwa wanamichezo kwenye fani nyingine. Kilimanjaro Marathon ni mbio za
kimataifa, lazima tuwe na zawadi zenye kuvutia wanariadha wazuri. Tumeona jinsi gani ushiriki wa wanariadha mbalimbali maarufu ulivyoleta msisimko mkubwa katika mbio hizi, lazima tuendelee kuboresha,” alisema.
Mbio hizo za nyika zimedhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, Vodacom Tanazania pamoja na makampuni mengine nchini ikiwemo kampuni ya KK Security,Tanga Cement. Good Year, Kilimanjaro Water,Tanzanite One, DT Dobie Tanzania, TPC, New Africa Hotel na Keys Hotel, jumla ya shilingi milioni 22 zitashindaniwa na wanariadha mabimbali wanaotarajiwa kushiriki katika mbio hizo

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment