Nahodha wa Chelsea John Terry atakosa mchezo wa Jumamosi wa kombe la FA dhidi ya Cardiff akiwa anachukua mapumziko ya siku chache kufuatia tuhuma za maisha yake ya faragha.
Terry alicheza siku ya Jumatano ambapo Chelsea walibugizwa mabao 2-1 na Everton.
Meneja wa Chelsea Ray Wilkins amesema John amepewa siku chache za kupumzika na hatocheza siku ya Jumamosi.
Terry alipanda ndege siku ya Alhamisi akielekea Dubai kumtembelea mkewe Toni, ambaye amekuwa nchini humo na wanawe kuepuka vyombo vya habari.
Terry, mwenye umri wa 29, wiki iliyopita alipokonywa unahodha wa timu ya taifa ya England baada ya madai alikuwa na uhusiano na Vanessa Perroncel, msichana aliyekuwa rafiki wa mchezaji wa zamani wa Chelsea Wayne Bridge.

0 comments:
Post a Comment